Kama unataka kushinda mikeka ya kubet na kupata pesa nyingi zingatia Kanuni 10 Muhimu zifuatazo;
Kanuni ya 1:
Tafuta kampuni inayotoa huduma nzuri. Hii ni kanuni muhimu katika soko la mikeka. Ikiwezekana jiunge na makampuni mengi yanayoendesha ubashiri wa michezo mitandaoni (bookmakers/betting sites) kadiri uwezavyo ili mradi tu uwe umetimiza masharti yao. Hii itakusaidia kufanya chaguzi na kujua ni kampuni ipi inatoa huduma nzuri na odds nzuri zinazoweza kukupatia wewe faida kubwa. Kwa sababu wakati mwingine unakuta makampuni yanatofautiana katika upangaji wa odd zao. Using’ang’anie kampuni moja tu eti kwa sababu ndiyo umeizoea labda kama wanakupatia huduma nzuri inayokuridhisha.
Kanuni ya 2:
Panga kiwango cha kuweka (mzigo). Baada ya kupata kampuni unayoona inafaa hatua inayofuata ni kujua kiwango gani unaweka kwa mkeka wako au utakachokuwa unatumia kuweka katika mikeka yako. Suala hili mara nyingi lina amuriwa na namna gani unajiamini katika kupanga mikeka yako (ubashiri wako) na faida unayoipata au tarajia kuipata. Kama hujawa mzoefu katika soko hili la mikeka usiweke kiwango kikubwa ambacho ikitokea umepoteza usiumie sana, labda uwe umeamua kujitoa muhanga (kujilipua) kwamba liwalo na liwe ama una uhakika/unajiamini na mkeka/mikeka yako.
Kanuni ya 3:
Usiwe na papara au haraka. Unaweza ukawa umepigwa kwenye mikeka mingi na unataka kurudisha pesa yako kwa haraka unaona ligi kubwa zinachezwa leo ukakimbilia kuchagua timu kubwa kubwa na kuweka kiwango kikubwa ili faida yako irudi haraka; usijaribu kufanya hivyo. Tulia panga mkeka wako taratibu kwa umakini kama ulivyozoea, ikiwezekana acha kuweka mkeka kwa muda ujipange na kufikiria vizuri ndio urudi mchezoni. Ama wakati mwingine michezo inakaribia kuanza unakimbizana na muda kuweka timu unazoziaminia; usifanye hivyo pia.
Kanuni ya 4:
Panga mkeka wa timu chache. Inatokea mara chache mtu kuweka timu nyingi kwenye mkeka mmoja na matokeo yote yakawa sahihi hata kama timu zote ni kubwa na unaziaminia huwa inatokea hata timu moja tu inakuangusha. Ingawa inashawishi kuweka timu nyingi kwenye mkeka mmoja kwani huwa inakuja faida kubwa lakini uhakika wa wewe kushinda pia unapungua tofauti na ukiwa umeweka timu chache, ingawa inatokea wakati mwingine hata kwa timu chache inatokea moja inakuangusha. Lakini ni bora badala ya kuweka timu nyingi kwa mkupuo kwenye mkeka mmoja unaweza kuzigawa hata kwenye makundi mawili au matatu ili kujiongezea nafasi ya kushinda.
Kanuni ya 5:
Fuatialia habari za michezo unayopenda kuiwekea mikeka. Kama ni mpira wa miguu, kikapu, n.k. jaribu kuzifuatilia habari za michezo hiyo au hata kuwa unaangalia mara kwa mara kujua uwezo wa timu na aina ya ligi mbali mbali. Hii itakusaidia kujua kama wachezaji muhimu wa timu hawapo uenda wapo majeruhi au wapo nje kwa adhabu au wamehama, pia unaweza kujua historia za timu zinazokutana. Unaweza kukuta timu A inaongoza ligi na timu G inakaribia kushuka daraja lakini ukiangalia historia ya timu hizi mbili zikikutana huwa inakuwa ngumu kwa timu A kuifunga timu G kirahisi, kwa hiyo kama wewe ni mfuatiliaji itakusaidia kufanya maamuzi mazuri katika kupanga mkeka wako.
Kanuni ya 6:
Chagua aina ya mkeka unaoweka kwa makini. Kuna wengine wanapenda kubet magoli, wengine matokeo ya kipindi cha kwanza tu, wengine matokeo ya vipindi vyote (HT/FT), wengine matokeo ya mchezo wote n.k. Kwa hiyo inakupasa kuchagua kwa makini aina mkeka unaotaka kuweka sio tu kuangalia sehemu utakayopata faida kubwa. Na hapa kufutilia michezo na kuzijua timu unazozibashiria kuna saidia sana, kwani unaweza kukuta timu A na G huwa hazifungani magoli mengi au lazima kila timu ipate goli zikikutana kwa hiyo ukaamua kubet magoli.
Kanuni ya 7:
Kuwa na staha. Usiwe na tamaa ya kutaka kupata faida kubwa kwa mara moja ni hatari sana kwani inaweza kupelekea ukawa unapata hasara kila siku. Cheza kwa kiasi na wakati mwingine unapoona kwamba mambo hayaendi vizuri unaweza ku