![]() |
Mbwana Samatta anaongoza kwa magoli ligi kuu Ubelgiji na Cardiff wanamtaka. |
- Cardiff City wameweka wazi nia yao ya kumuhitaji mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta
- Samatta kwa sasa ndio anayeongoza kwa ufungaji magoli kwenye ligi kuu ya Ubelgiji na pia alikuwa anatakiwa na Schalke
- Cardiff pia ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Nantes Emiliano Sala kuhusu usajili.
kwa mujibu wa habari kutoka Mail Online nchini Uingereza, Klabu ya Cardiff City inayoshiriki ligi kuu England imeonesha nia ya kumuhitaji mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta ambaye ndiye anayeongoza kwa ufungaji kwenye ligi kuu nchini Ubelgiji.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa anahusishwa na kujiunga na Schalke ya nchini Ujerumani lakini dili hiyo imebidi kusubiri baada ya Cardiff kuweka mezani ofa kiasi cha £13m.
Mshambuliaji huyo raia wa Tanzanian mpaka sasa ameifungia Genk jumla ya magoli 57 katika mechi 142 ndani ya misimu minne.
Samatta alijiunga na Genk akitokea klabu ya TP Mazembe ya nchini Kongo mwaka 2016, lakini alianza maisha yake ya soka kwenye klabu ya Simba SC nchini Tanzania.
Samatta, alizaliwa Dar Es Salaam, ameifungia timu ya taifa ya Tanzania magoli 17 katika mechi 45 tangu alipoanza kuitwa kwenye kikosi hicho cha Taifa akiwa na umri wa miaka 18.
Lakini pia Cardiff bado wapo kwenye mazungumzo kumsajili mshambuliaji wa Nantes Emiliano Sala ambaye anaweza kuwagharimu £20m.
![]() |
Cardiff pia wanaendelea na mazungumzo na mshambuliaji wa Nantes Emiliano Sala . |